News: Makau ashinda mbio za Frankfurt

Watch KTN Streaming LIVE from Kenya 24/7 on http://www.ktnkenya.tv
Mwanariadha anayeshikilia rekodi ya dunia katika mbio za marathon, patrick makau ameshinda mbio za frankfurt mapema leo mbele ya deressa chimsda kutoka ethiopia na gilbert kirwa kutoka kenya.makau ambaye alikuwa akishiriki katika mbio za kwanza tangu aprili mwaka huu alipokosa kumaliza mbio za london hakuwa miongoni mwa walioongoza lakini watangulizi wake walijipata matatani katika kilomita tano za mwisho. Makau ambaye aliwaambia waandishi wa habari baada ya mbio hizo kwamba hakuwa na nguvu mwanzo katika mashindnao haya alijipa moyo na kuwapita wapinzani wake. Muda wake wa saa mbili, dakika sita na sekunde nane ulikuwa dakika tatu nyuma ya rekodi yake ya saa mbili dakika tatu.chisma alikuwa wa pili mbele ya kirwa. Meselech melkamu alishinda mbio za kina dada baada ya kutumia muda wa saa mbili, dakika 21 na sekunde moja. Georgina rono akamaliza wa pili kisha daska mamitu akawa wa tatu.

Category: News
About The Author
-